Genesis 3:1-2

Kuanguka Kwa Mwanadamu

1 aBasi nyoka alikuwa mwerevu kuliko wanyama wote wa porini ambao Bwana Mungu aliwafanya. Nyoka akamwambia mwanamke, “Ati kweli Mungu alisema, ‘Kamwe msile matunda ya mti wowote wa bustanini’?”

2 bMwanamke akamjibu nyoka, “Tunaweza kula matunda ya miti iliyoko bustanini,
Copyright information for SwhNEN